FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Saturday, April 22, 2017

Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limetoa angalizo kuchukulliwa tahadhari zaidi kupambana na ugonjwa wa ini.
Katika ripoti yake ya kwanza ya dunia kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo, WHO imesema idadi kubwa ya watu kufariki kutokana na ugonjwa wa ini ambao unaweza kutibika unaosababishwa na matumizi ya pombe na dawa, inaongezeka.
Ugonjwa wa ini unaaminika kupoteza maisha ya watu 1.34 million mwaka 2015, idadi sawa na ile ya waliokufa kwa TB na UKIMWI, lakini wakati vifo vitokanavyo na UKIMWI na TB vikipungua, vifo vitokanavyo na ugonjwa wa ini vinaongezeka – ambapo vimeongezeka kwa 22% tangu kuanza kwa karne hii huku zaidi ya watu 325 million ambao wameathirika na ugonjwa huo hawajui kuwa wana virusi vya ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan amesema: “Ugonjwa wa ini sasa ni changamoto kubwa kwa afya ya jamii ambapo inahitaji juhudi za makusudi.”
VIDEO: Wizara ya Afya yatoa tamko kuhusu ugonjwa wa ZIKA Tanzania. Bonyeza play kutazama.

Monday, April 17, 2017


Kwa kufanya tafiti mbalimbali juu ya masuala ya viumbe hai na tabia zao, ndipo tunapata kufahamu namna viumbe walivyokuwa tofauti katika tabia na mienendo hata maumbile ambapo miongoni mwa mambo hayo hushangaza, hufurahisha, hustaajabisha lakini yakiwa na mafunzo kwa wanaoyafuatilia.
Unaambiwa Mende akigusana na binadamu hukimbilia sehemu yenye usalama kwake na kujisafisha. Hii ni kwa sababu huamini hakuna kitu au mtu safi kwake. Nimekukusanyia hapa chini list ya mambo saba ambayo huenda ulikuwa huyafahamu.

Monday, January 2, 2017Mtoto Maimuna Yahaya anahitaji msaada wako


 Mtoto Maimuna Yahaya akiwa  na Mama yake Mzazi  Tunu Juma.  Msaada unahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum  ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili. Yeye anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo.
Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu Juma Maziku amesema amekuwa akimpeleka mwanae huyo Maimuna katika hospitali ya KCMC kwa muda wa miaka 11. Hali ya mtoto inaendelea kuimarika, anaweza kukaa na anaweza kuongea. Bi. Tunu amekuwa akimpeleka mwanae huyu shule na kumsubiri hadi wamalizapo masomo ya siku na kumrejesha nyumbani kwa muda wa miaka miwili. Bi. Tunu Juma Maziku  anasema kwa sasa hali yake ya kiuchumi si nzuri, anashindwa kumpeleka mwanae kuhudhuria matibabu KCMC, hivyo anaomba msaada wa kifedha kwa wasamalia wema ili mtoto wake aendelee na matibabu.   Mahali wanapopatikana: Lushoto Mabwawani    Mawasiliano: Namba ya simu ya mama mzazi:+255712504768 Namba ya Tigo Pesa imesajiliwa kwa Jina la Maimuna Yahaya +255655779345 na Namba ya Airtel Money ni 0787204160 ,au namba ya halopesa imesajiliwa kwa jina la MWINYI MOHAMEDI imesajiliwa kwa jina la Tunu Juma. 

Msaada wa Matibabu kwa Mtoto Maimuna Yahaya (11)

   Pichani ni Mtoto Maimuna Yahaya  Mtoto Maimuna Yahaya akiwa na Mama yake Mzazi  Tunu Juma  **********************
Msaada wa Matibabu kwa mtoto Maimuna Yahaya Mtoto Maimuna Yahaya (11) anayesoma shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalum (wenye ulemavu) ya Irente Rainbow (Lushoto- Tanga) Darasa la pili, anasumbuliwa na tatizo la mifupa na ukubwa wa kichwa tangu kuzaliwa kwake, tatizo lililompelekea kuwa na ulemavu wa viungo na mtindio wa Ubongo. Mama wa mtoto huyo, Bi. Tunu...

Wednesday, December 21, 2016

Watafiti wanasema mwanamke anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni ya oestrogen huongezeka sana na pia mwili wake kubadilika hata hivyo, si wataalamu wengi walikuwa wamechunguza mabadiliko kwenye ubongo.
Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na Leiden walichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye ubongo. Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience.
Wanasayansi hao wanasema ujauzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi ya sehemu za ubongo wa mwanamke ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi na mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama ambapo hubadilisha ubongo wa mwanamke kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Uchunguzi ulifanywa kwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo, lakini hata hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke kuweka kumbukumbu.