FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Monday, May 29, 2017

R.I.P: Walichoandika mastaa Bongo miaka minne tangu Mangwea afariki


May 28 ni kumbukumbu ya kifo cha Mfalme wa Freestyle kutoka Bongo Albert Mangwea ambaye May 28, 2017 ametimiza miaka minne tangu afariki. Watu mbalimbali wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuandikia sala zao pamoja na namna walivyomfahamu Mangwea.
Taarifa za kifo cha Albert Mangwea zilisambaa mchana wa May 28, 2013 ambapo kulingana na ukubwa wa jina lake Tanzania hakuna aliyekuwa tayari kuamini kama ni kweli amefariki lakini baadaye ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.
Producer P Funk Majani alipost Picha 12 mfululizo za kukumbuka kifo cha Ngwea na kuandika: You will never be forgotten brother 🙏🏽”  (Hautasahaulika milele kaka 🙏🏽)

Saturday, April 29, 2017

Ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na wengi hasa wapenzi wa mchezo wa ngumi duniani, imewadia ambapo tambo na majigambo ya nani ni nani yatafika mwisho baada ya pambano la ngumi lililokuwa linatajwa kwa muda mrefu kumalizika.
Ni usiku wa Jumamosi April 29, 2017 katika uwanja wa Wembley jijini London kutashuhudiwa pambano kali la ndondi litakalowakutanisha miamba wawili kutoka Uingereza na Ukraine, Anthony Joshua vs Wladimir Klitschko.
Kuelekea pambano hilo kumekuwa na tambo nyingi kutoka kwa mabondia hao ambao kila mmoja ametamba ataibuka kidedea dhidi ya mwenzie. Na kwa kuwa nafahamu nina watu wanaoupenda mchezo huo, basi hizi hapa baadhi ya dondoo muhimu kuzifahamu kuelekea mchezo huo. Pambano hilo litapigwa mbele ya mashabiki wanaokadiriwa kufikia 90,000 katika uwanja wa Wembley mjini London.
Umri
Antony Joshua ana umri wa miaka 27 wakati mpinzani wake  Wladimir Klitschko ana umri wa miaka 41, ikiwa namaana kuwa anapanda ulingoni akiwa amezidiwa miaka 14 na mpinzani wake lakini wa urefu sawa wa futi 6 na inchi 6.
Kiasi cha fedha watakachopata
Kwa mujibu wa The Sun, pambano hili litawaingizia fedha kiasi cha pound 15 million kila mmoja bila kujali kushinda au kupoteza na ni pambano ambalo linakadiriwa kuvunja rekodi ya kuingiza watazamaji wengi zaidi Uingereza huku likitarajia kuingiza zaidi ya paundi 50 million – na kulifanya pambano ghali zaidi Uingereza.
Mapambano waliyocheza
Wladimir Klitschko anaingia ulingoni akiwa amecheza mapambano 68 ambayo ameshinda mapambano 64 huku mapambano 53 akishinda kwa ‘KO’. Hii ina maana kuwa amepoteza mapambano manne pekee huku pambano la mwisho kupoteza ilikiwa 2015 dhidi ya Tyson Fury ambalo alipoteza kwa pointi baada ya round 12. Hii ni baada ya kujiunga na ngumi za kulipwa baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic 1996 mjini Atlanta.
Kwa upande wa Antony Joshua tangu alipotwaa medai ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic London mwaka 2012 alijiunga rasmi na ndondi za kulipwa ingawa hajacheza mapambano mengi – amepigana mara 18 ambapo ameshinda yote kwa KO.

Saturday, April 22, 2017

Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limetoa angalizo kuchukulliwa tahadhari zaidi kupambana na ugonjwa wa ini.
Katika ripoti yake ya kwanza ya dunia kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo, WHO imesema idadi kubwa ya watu kufariki kutokana na ugonjwa wa ini ambao unaweza kutibika unaosababishwa na matumizi ya pombe na dawa, inaongezeka.
Ugonjwa wa ini unaaminika kupoteza maisha ya watu 1.34 million mwaka 2015, idadi sawa na ile ya waliokufa kwa TB na UKIMWI, lakini wakati vifo vitokanavyo na UKIMWI na TB vikipungua, vifo vitokanavyo na ugonjwa wa ini vinaongezeka – ambapo vimeongezeka kwa 22% tangu kuanza kwa karne hii huku zaidi ya watu 325 million ambao wameathirika na ugonjwa huo hawajui kuwa wana virusi vya ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan amesema: “Ugonjwa wa ini sasa ni changamoto kubwa kwa afya ya jamii ambapo inahitaji juhudi za makusudi.”
VIDEO: Wizara ya Afya yatoa tamko kuhusu ugonjwa wa ZIKA Tanzania. Bonyeza play kutazama.

Monday, April 17, 2017


Kwa kufanya tafiti mbalimbali juu ya masuala ya viumbe hai na tabia zao, ndipo tunapata kufahamu namna viumbe walivyokuwa tofauti katika tabia na mienendo hata maumbile ambapo miongoni mwa mambo hayo hushangaza, hufurahisha, hustaajabisha lakini yakiwa na mafunzo kwa wanaoyafuatilia.
Unaambiwa Mende akigusana na binadamu hukimbilia sehemu yenye usalama kwake na kujisafisha. Hii ni kwa sababu huamini hakuna kitu au mtu safi kwake. Nimekukusanyia hapa chini list ya mambo saba ambayo huenda ulikuwa huyafahamu.