FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Friday, September 13, 2013


Msanii wa filamu ambaye hivi karibuni alipata jeraha kubwa mkononi baada ya kupigwa chupa na mdada aitwaye Yvonne, Aunt Ezekiel (pichani) inadaiwa licha ya kidonda kuwa katika hali mbaya, amekuwa akionekana kwenye viwanja ya kula bata akijiachia kama kawa.
Mtu wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake aliliambia Ijumaa kuwa, msanii huyo amekuwa akisema licha ya kidonda alichonacho hawezi kukaa nyumbani wakati wenzake wakienda kujirusha.

“Ni kweli kidonda chake bado hakijapona vizuri lakini Aunt si mtu wa kukaa nyumbani, kujirusha ni kama kawa ila tumekuwa…HABARI KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.

“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.

“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu…
Na Jelard Lucas
MREMBO anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo (pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini, kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
Gazeti hili liliwasiliana na Jokate kuhusiana na maandiko hayo ambaye alijibu; “Hahaha….sina comment hapo aisee…”
Jokate pia ni mwanamitindo, msimamizi wa shughuli mbalimbali katika kampuni yake ya Kidoti iliyozinduliwa mwaka jana. HABARI KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

Mbowe afunguka

 AZUNGUMZIA HOJA YAKE ILIYOZUIWA, IKAZUA MASUMBWI BUNGENI
ALISIMAMA kutoa hoja, hakupewa fursa; akaambiwa akae chini. Hakukaa. Akaambiwa atoke nje; hakutoka. Wakaitwa askari kumtoa kwa nguvu, ukazuka mzozo uliozaa masumbwi bungeni.
Ni kauli gani ambayo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alitaka kutoa?
Vyanzo vyetu vya habari vilivyo karibu na Mbowe vilimnukuu jana akisema alichotaka kusema, akazuiwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ni hiki hapa:
“Kwanza, nilichotaka kusema ni kutoa hoja ya kuomba shughuli za Bunge zisitishwe kwa muda ili Kamati ya Uongozi ya Bunge ijadili makandokando yote ambayo yalikuwa yametokea juu ya muswada huo, ukiwamo uongo wa mwenyekiti wa kamati ya Bunge, uongo wa serikali bungeni na masuala mengine yote, ili sasa Bunge lipate mwelekeo chanya juu ya muswada huo na mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa masilahi ya wananchi.
“Hivyo hoja yangu ilikuwa muhimu sana kusikilizwa, ili viongozi wakutane kuokoa jahazi na kuondoa sintofahamu ambayo hatimaye imesababisha mjadala mkubwa na muswada mbovu kupitishwa bungeni kwa masilahi ya upande mmoja wa CCM,” Mbowe alikaririwa akisema.
Vyanzo hivyo vilisema kuwa kama Ndugai angemsikiliza Mbowe, hakuna fujo ambazo zingeibuka bungeni. Badala yake, naibu spika huyo alitumia ubabe kumlazimisha Mbowe akae chini, na baadaye akamwitia askari wamtoe, jambo ambao wabunge wengine wa upinzani walilikataa, wakajitoa mhanga kumlinda Mbowe.
Katika sakata hilo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, alivuliwa viatu na askari wapatao watano, wakambebea mzobemzobe hadi nje, huku mmjoa wao akisemekana kumuumiza kwa ngumi, jambo ambalo lilisababisha hasira za mbunge huyo naye akathubutu kumpiga konde askari huyo.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kama Ndugai angemsikiliza Mbowe, viongozi wa Bunge wangekutana na kuweka mazingira ya mjadala wenye hoja zenye afya kwa ajili ya masilahi ya Watanzania.
Vyanzo hivyo vinasema suala la Kiongozi wa Upinzani Bungeni kupewa nafasi kusema anaposimama hufanyika kwa mujibu wa kanuni ya 5(1) inayosema:
“Katika kutekeleza majukumu yake, yaliyotajwa katika ibara ya 84 ya Katiba, Spika ataongozwa na kanuni na pale ambapo kanuni hazikutoa muongozo, basi Spika atafanya kazi kwa kuzingatia Katiba, sheria za nchi, kanuni zingine zilizopo, maamuzi ya awali ya maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa Bunge la Tanzania.”
Kwa kuzingatia kanuni hii, na kwa kuwa Bunge letu linafuata utaratibu wa mabunge ya Jumuiya ya Madola (Westminster Model) ambao unatoa nafasi ya pekee kwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani anaposimama kutaka kusema jambo bungeni, makundi kadhaa ya wananchi yamekuwa yakimlaumu Ndugai kwamba alipaswa kumhukumu Mbowe baada ya kusikiliza hoja yake.
“Angempa nafasi ya kusema au kusikilizwa kwanza ili ajue kiongozi mwenzake alitaka kusema nini au alikuwa na jambo gani zito au la dharura ambalo lingeweza hata kusaidia Bunge zima, hivyo wananchi kunufaika,” kilisema chanzo kimoja cha karibu na Mbowe.
Mbowe alisema kuwa Ndugai anapaswa kuelewa kuwa bungeni ni mahali ambapo panapaswa kuheshimiwa kwa mijadala mikali, yenye hoja za afya kwa ajili ya masilahi ya wananchi, kwani moja ya kigezo muhimu katika uvumilivu wa kujadiliana ni kusikiliza, lakini hakutoa fursa hiyo kwa sababu anazozijua.
Duru za siasa zinaeleza kuwa Ndugai alilifanya kwa makusudi kumzuia Mbowe kwa sababu ya maelekezo yaliyotokana na vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vilivyoketi hivi karibuni jijini Dodoma.

No comments: