FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Thursday, October 10, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.
Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba…
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.
Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku ya Alhamisi.
Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.
Serikali inawataka wamiliki wa vyombo habari nchini kuwa na utamaduni wa kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA, kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI.
Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa ilivyoanisha.
Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013

No comments: