FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Tuesday, November 12, 2013

MAREHEMU NYAWANA FUNDIKIRA KUZIKWA NYUMBANI KWAO TABORA KESHO

Mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana.
MTANGAZAJI na mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana, atazikwa mjini Tabora.

Safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Tabora inategemewa kuanza kati ya saa 10 na saa 11 leo alasiri.
Mwili wa Nyawana ambao uko chumba cha kuhifadhia Hospitali ya Mwananyamala, unatarajiwa kuchukuliwa muda wowote kuanzia saa 7 kwaajili ya kwenda kuoshwa msikitini kabla haujapelekwa nyumbani kwao Magomeni Makanya (jirani na Bibi Nyau) ambako ndipo msiba  ulipo.   
Nyawana ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Tabora kunako mwaka 1986, alizaliwa jijini Dar es Saaam miaka 36 katika…
Mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana.
MTANGAZAJI na mwimbaji wa Taarab, Nyawana Fundikira (pichani) aliyefariki jana mchana, atazikwa mjini Tabora.
Safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Tabora inategemewa kuanza kati ya saa 10 na saa 11 leo alasiri.
Mwili wa Nyawana ambao uko chumba cha kuhifadhia Hospitali ya Mwananyamala, unatarajiwa kuchukuliwa muda wowote kuanzia saa 7 kwaajili ya kwenda kuoshwa msikitini kabla haujapelekwa nyumbani kwao Magomeni Makanya (jirani na Bibi Nyau) ambako ndipo msiba  ulipo.   
Nyawana ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Tabora kunako mwaka 1986, alizaliwa jijini Dar es Saaam miaka 36 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Msanii huyo aliyepitia vikundi vya Kings Modern Taarab na Tanzania Moto Modern Taarab alitamba zaidi akiwa kama msanii wa kujitegemea (solo artist) huku wimbo uliomtambulisha ukijulikana kama “Nipo Kamili Nimejipanga” uliotoka mwaka 2011 utunzi wake Thabit Abdul.
Wimbo wake wa pili ulijulikana kama “Umesharoga Wangapi” wakati wimbo wake wa mwisho aliouachia hivi karibuni ulikwenda kwa jina la “Shetani Kataja jina”.
Nyawana anategemewa kuzikwa kesho Jumatano mjini Tabora, sehemu ambayo inaaminika alijizolea umaarufu mkubwa zaidi kwa kazi yake ya utangazaji na baadae uimbaji.
Kimahusiano, Nyawana alifunga ndoa na mdau mkubwa wa taarab Kaisi Mussa Kaisimmiezi kadhaa iliyopita.
Akiongea jana mchana Hospital ya Mwananyamala wakati wa kwenda kuhifadhi mwili wa marehmu, mumewe Kasi Mussa alisema siku zote mkewe alikuwa akimweleza kuwa iwapo atatangulia kufariki basi mwili  wake ukazikwe Tabora.
Mara nyingi sana alikuwa akiirudia hii kauli, wakati mwingine hata tukiwa katika hali ya furaha na kutaniana lakini bado aliingiza hiyo kauli,” alisema Kaisi Mussa Kaisi. source global publishers

No comments: