FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Thursday, December 5, 2013

Katika tamasha maalum la Siku ya Ukimwi Duniani lililofanyika Desemba Mosi, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Lulu akiwa miongoni mwa waliohudhuria, alikiri kupima virusi vya ugonjwa huo mara kwa mara na kuwataka vijana wengine waige mfano wake.
“Vijana wengi waoga kujitokeza kupima Ukimwi, wanadhani kwa kufanya hivyo ni kujitafutia hofu ya kifo kitu ambacho si kweli.
“Hata mimi nilikuwa muoga sana lakini baada ya kupata elimu stahiki juu ya umuhimu wa kujua afya kila mara, nimekuwa nikipima mara kwa mara, hivyo hata ninyi nawaasa mjenge tabia ya kupima Ukimwi mara kwa mara,” alisema Lulu.
Baadhi ya wadau walihoji kulikoni msanii huyo mwenye historia mbaya huko nyuma, hasa ya starehe awe na tabia hiyo ya kupima Ukimwi mara kwa mara?
Wengi walihoji je amekuwa akipima mara kwa mara kwa sababu huwa anabadilisha wanaume mara kwa mara? Wengine walihoji amekuwa hatumii kinga?
“Kwa nini amekuwa na tabia ya kupima Ukimwi mara kwa mara? Ina maana huwa hatumii kinga? Au ni uaminifu mdogo katika uhusiano?” alihoji mdau mmoja ambaye pia ni msanii mkubwa wa filamu za Kibongo akiomba kusitiriwa jina.
Juzi paparazi wetu alilazimika kumsaka Lulu ili azungumzie kwa kina juu ya mjadala huo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

No comments: