FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790

FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
FOR ADVERTISEMENT CALL +255714890790
GREEN WORLD HEALTH CENTER;WATAALAAMU SHIRIKA LA KIMAREKANI LA GREEN WORLD WANAFANYA UPIMAJI WA AFYA NA UCHUNGUZI WA MAGONJWA SUGU KWA KUTUMIA VIPIMO VYA KISASA TUNAFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA MBALIMBALI MBALI NA TIBA ZAKE KAMA VILE VIDONDA VYA TUMBO KISUKARI MATATIZO YA INI MOYO NA FIGO FIBROIDS TB PUMU MAUMIVU YA VIUNGO NGUVU ZA KIUME KUWAHI KUFIKA KILELENI UZAZI SICKLECELL NA MAGONJWA MENGINE MENGI PIA TUNAPUNGUZA UNENE NA VITAMBI NA TUNAONDOA SUMU NA MAFUTA MABAYA MWILINI KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISINI KWETU TUPO POSTA MPYA JENGO LA AAR CITY HEALTH CENTER GOROFA YA PILI AU AU TABATA AU SIMU NO 0688704637

avdertse here call +255714489790

avdertse here call +255714489790

Tuesday, January 14, 2014


MWISHO WA DUNIA WATAJWA

Posted by GLOBAL on January 14, 2014 at 6:00amComments 
Stori: Mwandishi Wetu na Mitandao

WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.…
Stori: Mwandishi Wetu na Mitandao
WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
Askofu Zakaria Kakobe.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali.
Mwadhama Polycap Kadinali Pengo.
Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene  na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni  wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea.

KANISA LA WALA NYASI LAIBUKA!

Posted by GLOBAL on January 14, 2014 at 6:00amComments 
Stori: Mwand

No comments: